Alhamisi 17 Julai 2025 - 00:10
Marafiki na maadui wafahamu kwamba, taifa la Iran halito shiriki kwenye uwanja wowote huku likiwa liaonesha upande dhaifu / Shingo ya mhalifu haipaswi kuachwa

Hawza/ Kiongozi wa Mapinduzi amesisitiza kwamba, marafiki na maadui wote wafahamu kuwa taifa la Iran halito shiriki kwenye uwanja huku likiwa liaonesha upande dhaifu, kisha akaongeza kwa kusema: Tuna vifaa vyote vinavyohitajika kama vile mantiki na nguvu ya kijeshi, hivyo basi, iwe katika uwanja wa kidiplomasia au wa kijeshi, kila mara tunapoingia kwa tawfiq ya Mwenyezi Mungu, tutaingia tukiwa na mikono iliyojaa mafanikio.

Kwa mujibu wa  Shirika la Habari la Hawza kutoka Tehran, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, asubuhi ya leo katika kikao na Raisi na viongozi waandamizi wa taasisi ya mahakama pamoja na maraisi wa mahakama zote nchini, sambamba na kuchambua kazi kubwa iliyofanywa na taifa la Iran katika vita vya kulazimishwa vya hivi karibuni na kushindwa kwa mahesabu na mipango ya wavamizi, aligusia umoja mkubwa wa taifa la Iran licha ya tofauti za mitazamo ya kisiasa na uzito wa kidini katika kulilinda taifa adhimu la Iran, na akasisitiza: "Wajibu wa kila mtu ni kulinda umoja huu wa kitaifa."

Mtukufu Ayatollah Khamenei alisema kuwa: Kazi kubwa ya wananchi katika vita vya siku 12 ilikuwa ya aina ya azma, irada na kujiamini kitaifa, kwa kuwepo hali ya kisaikolojia na utayari wa kukabiliana na nguvu kama ya Marekani pamoja na mbwa wake aliemfunga mnyororo, yaani utawala wa Kizayuni, ni jambo lenye thamani kubwa sana.

Yeye aliashiria kwa kurejea kumbukumbu zilizochapishwa na watu wa utawala wa Pahlavi kwamba hata kwa siri na katika mikutano ya faragha hawakuwa na ujasiri wa kuipinga Marekani, na akaweka wazi kiwa: Iran imeepukana na hali ile ya wakati huo kiasi cha kwamba imefikia mahali ambapo sio tu haina hofu na Marekani bali imekuwa ikiitia hofu Marekani yenyewe, na hali hii ya kisaikolojia pamoja na irada ya kitaifa ndicho kitu kinachoiinua Iran na kuifikisha kwenye matarajio yake makubwa.

Kiongozi wa Mapinduzi alisisitiza kwa mara nyingine tena kwamba: Marafiki na maadui waelewe kuwa taifa la Iran halitowahi kushiriki kwenye uwanja wowote kama upande dhaifu, kisha akasisitizavkwa kusema: Tuna vifaa vyote muhimu kama vile mantiki na nguvu ya kijeshi, hivyo basi, iwe ni katika medani ya kidiplomasia au ya kijeshi, kila mara tunapoingia, kwa tawfiq ya Mwenyezi Mungu, tutaingia tukiwa tumebeba nguvu kubwa.

Mtukufu Ayatollah Khamenei alisisitiza kuwa: Pamoja na kwamba tunauona utawala wa Kizayuni kuwa ni kansa na Marekani kuwa ni mhalifu kwa sababu ya kuunga mkono utawala huo, lakini hatujawahi kwenda kutafuta vita wala hatujawahi kuivamia vita kwa hiari; hata hivyo kila mara adui aliposhambulia, sisi tulijibu kwa kishindo na kwa nguvu.

Yeye alitaja sababu ya wazi ya jibu la Iran lililokuwa kali na thabiti dhidi ya utawala wa Kizayuni kuwa ni utawala huo kulazimika kukimbilia msaada wa Marekani, na akasema kuwa: Kama utawala wa Kizayuni usingepigwa na kugaragazwa chini na ungekuwa na uwezo wa kujilinda, usingekimbilia kwa Marekani kwa namna hii, lakini ulitambua kuwa hauwezi kuivumilia Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kiongozi wa Mapinduzi alilitaja pigo la kulipiza kisasi la Iran dhidi ya shambulio la Marekani kuwa ni pigo nyeti sana, na akaongeza kwa kusema: Kituo kilichoshambuliwa na Iran kilikuwa kituo nyeti mno cha Marekani katika eneo hili, na kila mara ambapo vikwazo vya habari vitakapoondolewa, itafahamika kuwa Iran ilitoa pigo kubwa kiasi gani, bila shaka, pigo kubwa zaidi ya hili linaweza pia kutolewa dhidi ya Marekani na wengine.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha